Msaada charity Association ilioko Dallas,USA.Imejitolea 100,000/- kusomesha Kijana Dido alioko Kidato cha kwanza Mamsa.
Hii ni baada ya Mwanafunzi huyu kufaulu katika mtihani wa kitaifa na hatimae kushindwa kusoma Shule ya upili kutokana na hali duni ya maisha yake,isitoshe kijana huyu ni yatima.
Ufadhili huu umesimamia mpaka sare zake za shule,vitabu na malazi.
Sura za bashasha zimeonekana kati ya Mwanafunzi huyo na waalimu kwa jumla kwa kupata kushirikiana na Chama hicho kufanikisha Gurudumu la Elimu.
Shukran za dhati kutoka Mamsa kwanzia Mwanafunzi,Waalimu,Wasimamizi na Familia yote kwa jumla.hakuna cha kuwalipa ila Mola ndie atwajazi kila la kheir na awape uwezo musaidie wengi wengine.
Ukurasa wetu wa Facebook
Tuesday, 27 January 2015
100,000/-Ksh kutoka Msaada Charity Association yasomesha yatima Mamsa 2015
Labels:
Schoolarship
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment